Google My Business

Google My Business ni huduma ya mtandaoni kwa wamiliki wa kampuni za biashara inayoendeshwa na Google. Huduma hiyo ilizinduliwa mnamo Juni 2014 kama njia ya kuwapa wamiliki wa kampuni za biashara uwezo zaidi wa kuamua habari gani zionekane mtu anapotafuta jina fulani la biashara kwenye tovuti ya utafutaji ya Google. Huduma hiyo inawawezesha watu kuthibitisha taarifa za biashara zao kama vile jina, anuani, n.k. Biashara zilizojisajili kwenye Google My Business hutokea pia kwenye Google Maps. Inasaidia pia biashara ndogo kupata wateja kupitia mtandao kwa kuwa matokeo ya utafutaji huonyesha aina za biashara zinazotafutwa katika makazi ya mtafutaji. Maelezo ambayo hutokeza kwenye tovuti ya Google kutokana na huduma hiyo ni pamoja na saa za kufunguliwa kwa biashara, anuani, simu, na picha. Huduma hiyo hutolewa bure.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne